Naibu Waziri wa Maji Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Zawadi Amour Nassor amefanya ziara kisiwani pemba kupitia mirad ya ahueni ya UVIKO-19 iliyopo katika kisiwa hicho ili kuona tija iliyofikiwa na miradi hiyo katika kutatua changamoto za maji katika maeneo yaliyoainishwa kufikiwa na mradi.
Katika Ziara Yake Naibu Waziri alipitia miradi miwili ambao ni wa Chanjaani na Pujini Dodo yote ikiwa Wilaya ya Chake Chake Pemba, ambapo katika ziara hiyo aliambatana na Afisa Maendeleo ya Maji Pemba Ndug. Juma Masoud Juma na Afisa kutoka Mamlaka ya maji (ZAWA) Wilaya ya Chake chake Pemba.
Aidha, Naibu alibaini changamoto zilizokuwepo katika utekelezwaji wa utoaji huduma na kuwataka wananchi wawe na subra wakati utatuzi wa changamoto hizo ukiwa unatatuliwa ufumbuzi.
Nao wananchi wa maeneo hayo walimshukuru sana Naibu Waziri kwakuja na kufuatilia changamoto hizo na kuona kwamba ujio huo utapelekea ufumbuzi wa kudumu katika maeneo yaliyotakiwa kufikiwa.