The Revolutionary Government of Zanzibar

drop1

Core Functions


Majukumu ya Wizara ya Maji Nishati na Madini.

Miongoni mwa mjukumu ya Wizara ya Maji, Nishati na Madini ni kama yafuatayo:

 1. Kuendeleza na kusimamia utekelezaji wa sera na mipango ya kisekta
 2. Kuendesha na kuendeleza tafiti zenye uwiano na maendeleo ya sekta
 3. Kusimamia  utawala wa raslimali watu, fedha na rasilimali nyengine
 4. Kuendeleza, kusimamia na kudhibiti sekta za Maji, Nishati na Madini
 5. Kusimamia ujenzi, matengenezo na uendelezaji wa miundombinu ya maji.
 6. Kuhakikisha kuwepo kwa maji safi na salama mijini na vijijini.
 7. Kuhakiksha kuwepo kwa huduma nzuri za maji kwa wananchi.
 8. Kusimamia uendelezaji, matengenezo na ulinzi wa vyanzo vya maji pamoja na miundombinu.
 9. Kusimamia ujenzi na uendelezajii wa miundombinu ya nishati.
 10. Kuhakikisha kuwepo kwa huduma nzuri za umeme kwa wananchi.
 11. Kuratibu na kuendeleza juhudi za kuendeleza vynazo vya nishati mbadala
 12. Kupokea malalamiko ya wananchi na kuyafanyia kazi ipasavyo.
 13. Kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za nishati kwa wananchi
 14. Kuhakikisha kupatikana kwa mafuta kwa wananchi kwa muda unaotakiwa
Malengo Mkakati
 1. Kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa watumiaji wote wa maji kwa asilimia 95% maeneo ya mjini na 85%maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2020.
 2. Kuboresha mapato ya Serikali kwa ufanisi na kuzuia mianya ya upotevu wa fedha za Serikali.
 3. Kuhakikisha Zanzibar inakua na kiwango kizuri cha Nishati, Usalama wa Nishati na mfumo mzuri wa Usimamizi wa wa nishati ifikapo mwaka 2025.
 4. Kuendeleza Utawala Bora na kutoa huduma stahiki kwa wananchi wote.
 5. Kuboresha huduma za Umeme na kuandaa mazingira ya kuwavutia wawekezaji katika Nyanja za nishati mbadala.
 6. Kusimamia vizuri rasilimali za Mchanga, Vifusi na Kokoto ili ziweze kufaidisha wananchi wa Zanzibar na kuhakikisha tunaondoa tatizo la uhaba wa Rasilimali za Mchanga na Vifusi
 7. Kukuza mashirikiano ya kisekta baina ya Serikali na Sekta za Maji, Nishati na Madini.

NEWS

2

2