The Revolutionary Government of Zanzibar

drop1

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imetiliana saini na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) kuhusianana na Mradi wa Upembuzi yakinifu wa Maji.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Leo Aprili 13, 2022 imetiliana saini na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) kuhusianana na Mradi wa Upembuzi yakinifu wa Maji.
Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), tawi la Zanzibar.

Aidha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dr Saada Mkuya Salum, Naibu Waziri, Wizara ya Maji, Nishati na Madini Mhe. Shabani Ali Othman, Katibu Mkuu wa ORFM Dkt Juma Malik Akil, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Nishati na Maadini Dkt Mngereza Mzee Miraji na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dkt Salha Kassim Moh’d kwa upande wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani imewakilishwa na Mr. Johannes Sperrfechter na Madam Andrea Hoeltke.

Jumla ya Tsh 1.7 bilioni kutoka (KFW) zitatumika ktk Mradi wa Upembuzi yakinifu katika Sekt ya Maji Zanzibar (Unguja na Pemba).
Viongizi hao, wameeleza kuwa Mradi huu utafanya tathmini ya Miundombinu ya Maji safi na maji taka ili kubaini kiasi cha maji yaliyomo ardhini na namna ya kuyapata ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa Maji safi na salama Zanzibar.

Aidha, hatuna hii ya utiaji saini Kwa hati Za makubaliano utasaidia kwenye kutekeleza programu ya maji Maji (Zanzibar Water Investment Program) ambayo ilizinduliwa na Mheshimiwa DK Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mbali tarehe 11Machi 2022 katika Hoteli ya Melia, Kiwengwa Zanzibar. Mpango ambao unaenda kutekeleza na kutatua changamoto Za maji visiwani Unguja na Pemba Kwa mda wa miaka mitano 2022-2027

Imetayarishwa na Kitengo cha Uhusiano
Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar
13 Aprili, 2022

NEWS

2

2