The Revolutionary Government of Zanzibar

drop1

Uendeshaji na Utumishi

Idara hii itahusika na utoaji wa huduma za uendeshaji na utumishi, kusimamia maslahi ya rasilimali watu, pamoja na kutunza, kuhuisha na kuhifadhi kumbukumbu za Ofisi. Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi ambae ni mteuliwa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. 

Majukumu ya Idara 

 1. Kutoa huduma za uongozi wa Rasilimali watu na Utawala kwa Wizara;
 2. Kusimamia masuala ya ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi wa Wizara.
 3. Kuhakikisha kuwepo kwa watendaji wa kutosha na wenye sifa na kuweka kumbukumbu za masuala mbalimbali yahusuyo watendaji;
 4. Kufanya tathmini ya utendaji wa kila mtumishi wa Wizara na kuandaa ripoti ya hali ya utumishi kila baada ya muda kwa mujibu wa matakwa ya sheria au maagizo maalum;
 5. Kuratibu masuala Mtambuka yakiwemo (UKIMWI, jinsia, Mabadiliko ya tabianchi na mambo ya idadi ya watu); 
 6. Kuhifadhi na kutunza kumbukumbu zote za Wizara;
 7. Kusimamia rasilimali zote za Wizara;
 8. Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa mteja.
 9. Kushughulikia na kukadiria upatikanaji wa mahitaji, vifaa na vitendea kazi na kuhakikisha vinatunzwa na kutumika ipasavyo; 
 10. Kuandaa, kuhuisha na kusimamia utekelezaji wa mkataba wa utoaji wa huduma kwa umma;
 11. Kuandaa na kutunza kumbukumbu za watumishi;
 12. Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo na kuandaa mipango ya mafunzo;
 13. Kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi;
 14. Kutafsiri na kusimamia sheria, kanuni na miongozo ya kazi; na
 15. Kuratibu utekelezaji wa upimaji utendaji kazi.

NEWS

2

2