- Kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa watumiaji wote wa maji kwa asilimia 95% maeneo ya mjini na 85%maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2020.
- Kuboresha mapato ya Serikali kwa ufanisi na kuzuia mianya ya upotevu wa fedha za Serikali.
- Kuhakikisha Zanzibar inakua na kiwango kizuri cha Nishati, Usalama wa Nishati na mfumo mzuri wa Usimamizi wa wa nishati ifikapo mwaka 2025.
- Kuendeleza Utawala Bora na kutoa huduma stahiki kwa wananchi wote.
- Kuboresha huduma za Umeme na kuandaa mazingira ya kuwavutia wawekezaji katika Nyanja za nishati mbadala.
- Kusimamia vizuri rasilimali za Mchanga, Vifusi na Kokoto ili ziweze kufaidisha wananchi wa Zanzibar na kuhakikisha tunaondoa tatizo la uhaba wa Rasilimali za Mchanga na Vifusi
- Kukuza mashirikiano ya kisekta baina ya Serikali na Sekta za Maji, Nishati na Madini.